Swali: Serikali ya mji wetu imetukataza kuvaa Niqaab barabarani na mahala pengine pote hadharani, je inajuzu kwangu kumuomba mke wangu kufunika uso wake na kutoka wakati tu wa dharurah kwa kuzingatia ya kwamba akifanya hivyo anaweza kufungwa, na mimi siwezi kuhama…

al-Fawzaan: Kufungwa?

Muulizaji: Ndio.

Jibu: Sidhani kama utafungwa. Ambae anaweza kufungwa ni yule mwenye kuvuruga amani, mtu kama huyu anaweza kufungwa. Ama kwa yule asiyevuruga amani hawezi kufungwa. Na ni juu yenu kuwa na subira na kushikamana barabara na Dini yenu, na tafuta kinga kwa Allaah na kuweni na subira. Kama alivyosema Muusa (´alayhis-Salaam) kuwaambia watu wake:

قَالَ مُوسَى لِقَوْمِهِ اسْتَعِينُوا بِاللّهِ وَاصْبِرُواْ إِنَّ الأَرْضَ لِلّهِ يُورِثُهَا مَن يَشَاء مِنْ عِبَادِهِ وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ

“Muusa akawaambia watu wake: “Ombeni msaada kwa Allaah na subirini. Hakika ardhi ni ya Allaah. Naye humrithisha amtakaye katika wajawake. Na mwisho ni wa wachaji Allaah.” (07:128)

Wala hakuna haja ya mke wako kutoka barabarani. Abaki nyumbani.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alfawzan.ws/sites/default/files/tg–1431-5-27.mp3
  • Imechapishwa: 28/01/2024