Swali: Ni kipi unachowanasihi watu kuhusu uelewa juu ya swawm ya Ramadhaan?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule ambaye Allaah anamtakia kheri, basi humpa ufahamu katika dini.”

Ni lazima kwa waislamu wasome yale wasiyoyajua na wawaulize wanazuoni kuhusu yale yenye kuwatatiza. Ni mamoja mambo hayo yanahusiana na funga na mambo mengine. Allaah (Subhaanah) amesema:

فَاسْأَلُواْ أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لاَ تَعْلَمُونَ

“Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth Swahiyh:

“Yeyote mwenye kujulisha kheri, basi anapata mfano wa ujira wa mwenye kuifanya.”

“Yeyote asiyeacha maneno ya uwongo, kuyatendea kazi na ujinga, basi Allaah hana haja kwa yeye kuacha chakula na kinywaji chake.”

Kwa hivyo muumini anatakiwa kuuliza, awe na utambuzi na awe na uelewa katika dini ili ajue yale ambayo Allaah amemuwajibishia na yale aliyomuharamishia.

[1] 16:43

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/8652/اهمية-الفقه-في-احكام-صوم-رمضان
  • Imechapishwa: 13/03/2023