Swali: Mwanamke akila baadhi ya siku za Ramadhaan kutokana na udhuru unaokubalika katika Shari´ah. Wakati wa kulipa analazimika kulipa kwa kufululiza? Itasihi ikiwa atalipa kwa kuachanisha siku? Je, ni lazima kufunga siku sita za Shawwaal kwa kufuatanisha au kwa kuachanisha?

Jibu: Kulipa Ramadhaan ni lazima. Lakini sio lazima kufunga kwa kufuatanisha siku. Akifunga kwa kufuatanisha ndio bora zaidi na akiachanisha siku ni sawa. Kulipa ni lazima na kufululiza sio lazima. Akilipa deni la Ramadhaan kwa kuachanisha siku ni sawa. Haijalishi kitu aliacha kufunga Ramadhaan kutokana na ugonjwa, hedhi au damu ya uzazi. Kulipa deni hakulazimu kufuatanisha siku. Lakini inapendeza kufuatanisha. Mwanamke akilipa kwa kuachanisha siku ni sawa. Mwanamme pia anaweza kulipa deni lake kwa sababu aliacha kufunga Ramadhaan kwa sababu alikuwa mgonjwa. Baada ya hapo akafunga kwa kuachanisha. Hapana vibaya kufanya hivo.

Kuhusu kufunga siku sita za Shawwaal sio lazima kufunga. Ni Sunnah na inapendeza. Kufunga siku sita za Shawwaal sio lazima. Mwenye kuziacha hapana vibaya na mwenye kuzifunga anapata ujira.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4645/حكم-التتابع-في-قضاء-صوم-رمضان%C2%A0
  • Imechapishwa: 13/03/2023