27. Tofauti kati ya washirikina wa kale na wa sasa

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Msingi wa nne: washirikina wa zama zetu ushirikina wao ni wa khatari zaidi kuliko washirikina wa mwanzoni. Washirikina wa mwanzoni walikuwa wakifanya shirki katika kipindi cha raha, wakati katika kipindi cha shida walikuwa ni watakasifu katika ´ibaadah. Ama washirikina wa zama hizi ni wenye kufanya shirki katika kipindi chote, sawa iwe ni wakati wa raha au shida.

Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

فَإِذَا رَكِبُوا فِي الْفُلْكِ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ فَلَمَّا نَجَّاهُمْ إِلَى الْبَرِّ إِذَا هُمْ يُشْرِكُونَ

“Wanapopanda merikebu [wakakumbwa na misukosuko] basi humwomba Allaah kwa kumtakasia Yeye dini. Lakini anapowaokoa [kwa kuwafikisha salama] nchikavu, tahamaki hao wanamshirikisha.”[1]

Mwisho!

Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake.

MAELEZO

Kanuni hii inabainisha tofauti kati ya washirikina wa mwanzo na washirikina waliokuja baadaye. Makusudio ya washirikina waliokuja nyuma ni washirikina wakati wa Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah). Tofauti kati yao ni kwa njia nyingi:

1 – Washirikina wa mwanzo shirki yao ilikuwa nyepesi na washirikina waliokuja nyuma shirki yao ilikuwa kubwa zaidi, ingawa wote ni washirikina. Hata hivyo shirki inatofautiana kama ambavyo ukafiri pia unatofautiana. Allaah (Ta´ala) amesema:

الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ زِدْنَاهُمْ عَذَابًا فَوْقَ الْعَذَابِ بِمَا كَانُوا يُفْسِدُونَ

“Wale waliokufuru na wakazuia kutokana na njia ya Allaah, tutawazidishia adhabu juu ya adhabu kwa sababu ya ufisadi waliokuwa wakiufanya.”[2]

Shirki inatofautiana kama ambavyo wapwekeshaji wanatofautiana katika Tawhiyd na imani yao. Baadhi ya watu wana imani na Tawhiyd yenye nguvu zaidi na vivyo hivyo washirikina baadhi yao wana ushirikina mbaya na khatari zaidi.

Mshirikina ambaye anamuomba asiyekuwa Allaah ni mshirikina. Lakini ikiwa anamuomba asiyekuwa Allaah, anawaudhi waumini, anawafitinisha kutokana na dini yao na anawavuta kwenye ukafiri anakuwa mbaya zaidi. Mshirikina ambaye shirki yake inakomeka kwenye nafsi yake anahesabika ni mshirikina. Hata hivyo mshirikina ambaye anamshirikisha Allaah, anawaudhi waumini, anawafitinisha na kuwalazimisha kufanya shirki, anakuwa mbaya zaidi na mwenye adhabu maradufu. Allaah (Ta´ala) amesema:

الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ زِدْنَاهُمْ عَذَابًا فَوْقَ الْعَذَابِ بِمَا كَانُوا يُفْسِدُونَ

“Wale waliokufuru na wakazuia kutokana na njia ya Allaah, tutawazidishia adhabu juu ya adhabu kwa sababu ya ufisadi waliokuwa wakiufanya.”[3]

Kuna tofauti kati ya ambaye amekufuru tu kwa nafsi yake, hawaudhi wengine na wala hazuilii watu kutokana na njia ya Allaah na ambaye anawavuta watu kwenye ukafiri na pia anawaudhi, huyu ukafiri wake ni mkubwa na dhambi yake ni kubwa:

الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ زِدْنَاهُمْ عَذَابًا فَوْقَ الْعَذَابِ بِمَا كَانُوا يُفْسِدُونَ

“Wale waliokufuru na wakazuia kutokana na njia ya Allaah, tutawazidishia adhabu juu ya adhabu kwa sababu ya ufisadi waliokuwa wakiufanya.”

[1] 29:65

[2] 16:88

[3] 16:88

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah, uk. 151-152
  • Imechapishwa: 13/03/2023