26. Faida katika Hadiyth ya Abu Waaqid al-Laythiyy (Radhiya Allaahu ´anh)

Hadiyth imekusanya faida kadhaa ikiwa ni pamoja na zifuatazo:

1 – Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwakemea Maswahabah ambao wameomba shirki.

2 – Mwenye kuomba shirki na asitumbukie ndani yake hazingatiwi amefanya shirki.

3 – Anayetaka kufanya shirki na akaiomba kisha akakaripiwa na kukemewa ambapo akakomeka, hahesabiki ameingia ndani ya shirki.

4 – Kustaajabishwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maombi yao pale aliposema:

“Allaah ni mkubwa.”

5 – Maswahabah kuomba kwao shirki wamefuata nyayo za wana wa israaiyl kwa Muusa pale walipomwambia:

اجْعَل لَّنَا إِلَهًا كَمَا لَهُمْ آلِهَةٌ

“Tufanyie mungu kama ambavyo wao wako na miungu!”[1]

6 – Maneno ya Maswahabah – Abu Waaqid al-Laythiyy na wenzake – yanatofautiana na maneno ya wana wa israaiyl. Licha ya hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akayafanya ni yenye kulingana. Kinachozingatiwa ni ule uhakika na malengo na kinachozingatiwa sio matamshi.

7 – Shirki ya kutafuta baraka ni kule kuamini baraka kwenye mti na kuona kuwa una baraka, unanufaisha na kwamba wote uko na baraka.

8 – Hakuna tofauti na vile vinavyoabudiwa na kwamba anayemwabudu asiyekuwa Allaah (Ta´ala) ni mshirikina. Haijalishi kitu kile alichokiabudu; mti, jiwe, Malaika, Mtume au vyengine. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakutofautisha kati ya washirikina na akahalalisha damu na mali yao.

9 – Radd kwa waabudia makaburi ambao wanawaomba wafu badala ya Allaah, wanawawekea nadhiri na wanasema eti hawamshirikishi Allaah na kuwa eti wanashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, wanaswali, wanahiji na wanatoa zakaah. Hadiyth hii inawaraddi kwamba sio washirikina wote wenye kuabudu mizimu na makaburi. Bali baadhi yao wanawaabudu Malaika, wengine waja wema na wengine wanaabudu jua na mwezi. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakutofautisha kati yao na akahalalisha kuuliwa.

10 – Du´aa ni ´ibaadah na kuchinja ni ´ibaadah. Ukiwachinjia wafu hawa shahaadah yako imechenguka na swawm, swalah, hajj na matendo mengine yote yameporomoka. Mfano wa hilo mwenye kutawadha akafanya vizuri wudhuu´ wake na akajitwahirisha na kufanya vizuri twahara yake kisha ukachenguka wudhuu´ wake na akapata hadathi, swalah na ´ibaadah yake inaharibika. Miongoni mwao wako ambao wanawaomba wafu kama vile al-Husayn na ´Abdul-Qaadir na kuwaomba wawape utajiri na wawashike mkono, inaharibika shahaadah yao na ´ibaadah zao kama vile swalah, swawm, hajj na matendo yao mengine yote. Badala ya yeye kuwa muislamu anakuwa mshirikina.

[1] 07:138

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah, uk. 149-150
  • Imechapishwa: 13/03/2023