Swali: Je, imethibiti kuwa Israa´ na Mi´raaj ni usiku wa tarehe ishirini na saba katika mwezi huu – Sha´baan – na siku hiyo ina mambo maalum tofauti na siku zingine?

Jibu: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ametaja Israa´ katika Suurat-ul-Israa´ ili waislamu wamhimidi Allaah kwa neema hii kubwa ambayo Ameifanya kuwa maalum kwa Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni katika manufaa yao mpaka siku ya Qiyaamah. Kadhalika Mi´raaj, nayo ni kupandishwa kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka ardhini na kwenda mbinguni juu ya mbingu (ya saba) mpaka katika mkunazi wa mwisho akiwa pamoja na Jibriyl (´alayhis-Salaam). Hili limetajwa katika Suurat-un-Najm. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Ametaja Mi´raaj katika Suurat-un-Najm na Israa´ katika Suurat-ul-Israa´.

Hata hivyo, si Allaah wala Mtume Wake hawakubainisha hili lilitokea wakati gani. Kwa nini tujikalifishe na kufanya ni siku maalum katika mwaka au mwezi. Hili halina asli na wala halina dalili. Isitoshe, halina faida kwetu isipokuwa kuanzisha tu Bid´ah. Tunamuomba Allaah afya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo-24-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 03/05/2015