Laylat-ul-Qadr siku y 15 Sha´baan?

Hapakuthibiti fadhila yoyote katika usiku wa Nisfu Sha´baan inayotofautiana na masiku wala usiku wowote wa mwezi wa Sha´baan. Hapakuthibiti lolote katika hili.

Vilevile wanasema kuwa Laylat-ul-Qadr inakuwa katika usiku wa Nisfu Sha´baan, si kweli. Laylat-ul-Qadr inakuwa katika Ramadhaan. Kwa sababu Allaah (Ta´ala) Amesema:

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ

“Hakika Sisi Tumeiteremsha (Qur-aan) katika Laylatil-Qadr (usiku wa cheo).” (97:01)

Laylat-ul-Qadr inakuwa katika masiku kumi ya mwisho ya Ramadhaan. Hili ni kwa Ijmaa´. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaitafuta katika Ramadhaan na hakuwa anaitafuta katika mwezi wa Sha´baan. Wapi wametoa haya kwamba Laylat-ul-Qadr inakuwa katika usiku wa Nisfu Sha´baan.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo-24-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 03/05/2015