Imepokelewa kwamba kuna bwana mmoja alisema kumwambia al-Hallaaj:

“Nataka tufaha.” Na haikuwa msimu wake. al-Hallaaj akaashiria mkono wake juu, akampa bwana yule tufaha na akasema: “Tufaha hili ni kutoka Peponi.” Alipoambiwa kwamba tufaha ya Peponi haiozi ilihali tufaha yake iko na minyoo akasema: “Kwa sababu limetoka katika maisha ya milele na kuja katika maisha yatayotokomea. Ndio maana limepatwa na janga.”

Tazama karama za masikini huyu na mambo yenye kwenda kinyume na ada. Tunaomba ulinzi kwa Allaah kukoseshwa nusura. ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akimuomba Allaah ulinzi dhidi ya unafiki wa kunyenyekea.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/324-325)
  • Imechapishwa: 18/11/2020