Tonge la mwisho la kusindikiza adhaana

Swali: Ni lini inalazimu kujizuilia na chakula? Je, ni kabla ya adhaana ya Fajr au baada yake? Je, mtu anapata dhambi ikiwa anajizuila wakati anaposikia adhaana?

Jibu: Ikiwa anaona kuingia kwa alfajiri basi analazimika kujizuilia. Pindi kunapopambazuka alfajrii basi ni kama ambaye yuko jangwani anatakiwa kujizuilia pale anapoadhini muadhini. Kwa sababu muadhini hujichunga kwa kufuata hizi kalenda za sasa. Muadhini akiadhini basi ni lazima kujizuilia. Akila au akanywa kitu kidogo wakati ambapo muadhini anaanza adhaana hapana neno – Allaah akitaka. Lakini ajitahidi awe amemalizika daku yake kabla ya adhaana ili asiingie ndani ya shubuha. Lakini kukiadhiniwa na mkononi mwake kuna tonge au kinywaji hapana vibaya [akakitumia].

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/794/فتاوى-رمضانية
  • Imechapishwa: 01/04/2023