Swali: Naomba kujua tofauti kati ya shufwa na witr katika swalah ya usiku? Ni wajibu kukitilia nia kila kimoja?

Jibu: Shufwa ni pale anaposwali Rak´ah mbili na witr ni pale anaposwali Rak´ah moja, tatu, tano au saba. Zote hizi za mwisho huitwa kuwa ni witr. Shufwa ni pale anaposwali Rak´ah mbili, nne au sita. Hata hivyo kilichosuniwa ni yeye kutoa salamu kila baada ya Rak´ah mbili. Haijuzu kwake kukusanya Rak´ah nne, sita na nane kwa salamu moja. Anatakiwa kutoa salamu kila baada ya Rak´ah mbili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah ya usiku ni [Rak´ah] mbilimbili.”

Hata hivyo hapana vibaya akiswali witr Rak´ah tatu au tano. Hili ni lenye kuvuliwa. Vivyo hivyo mchana aswali Rak´ah mbilimbili. Imekuja katika upokezi mwingine:

“Swalah ya usiku na mchana ni [Rak´ah] mbilimbili.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/10653/الفرق-بين-الشفع-والوتر-في-صلاة-الليل
  • Imechapishwa: 06/04/2023