Tikitimaji kwa tende tosa

57- ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

”Alikuwa akila tikiti kwa tende tosa [na akisema: ”Tunavunja joto ya hii kwa baridi ya hii na baridi ya hii kwa joto ya hii.]”

Ameipokea al-Humaydiy (1/42), Abu Daawuud (3835), at-Tirmidhiy (1/338), Abu Bakr Muhammad bin ´Abdillaah al-Harawiy katika ”al-Fawaa-id” (Makhtuta 1/144), Abu Nu´aym katika ”Akhbaar Aswbahaan” (1/103) na katika ”at-Twibb” (17139), Abu Ja´far al-Bakhtariy katika ”al-Fawaa-id” (2/77/4) na Abu Bakr bin Abiy Daawuud katika ”Musnad ´Aaishah” (2/54) kupiti ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa). at-Tirmidhiy amesema:

”Hadiyth ni nzuri na geni.”

Cheni ya wapokezi ya al-Humaydiy ni Swahiyh na imeafikiana na sharti za al-Bukhaariy na Muslim. Cheni ya wapokezi ya Abu Daawuud ni nzuri na ziada ni yake. Haafidhw Ibn Hajar ameiegemeza kwa an-Nasaa´iy pasi na ziada na akasema:

”Cheni yake ni Swahiyh.”

Ibn-ul-Qayyim amesema baada ya kutaja ziada:

”Zipo Hadiyth nyingi kuhusu tikiti lakini zote hazikusihi isipokuwa Hadiyth hii peke yake. Inalenga tikitimaji. Ni yenye baridi, unyevu na yenye rotuba. Ni yenye kuteleza kwa wepesi kuliko tango. Ni nyepesi kubadilika pasi na kujali imechanganywa na kitu gani tumboni. Ikiwa yule mwenye kuila ni mwenye joto, basi ananufaika nalo sana. Na kama yuko na kibaridi, basi azuie madhara kwake kwa tangawizi kidogo na mfano wake. Tikiti inatakiwa kuliwa kabla ya chakula kwa ajili ya kuepuka kuhisi vibaya na kutapika. Baadhi ya madaktari wamesema kuwa tikiti kabla ya chakula inasafisha tumbo vizuri na kuondosha magonjwa.”[1]

Haya ambayo ameyanasibisha kwa baadhi ya madaktari yamepokelewa kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), lakini hata hivyo hayakusihi.

[1] Zaad-ul-Ma´aad (3/175).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (1/1/124-125)
  • Imechapishwa: 03/08/2020