Ee uchafu wa watenda madhambi!

هَـٰذَا مُغْتَسَلٌ بَارِدٌ وَشَرَابٌ

”Hii [chemchem ya] maji baridi ya kuogea na ya kunywa.”[1]

Watenda madhambi wanatakiwa kurejea katika vikao vya kielimu. Kinywaji cha mawaidha ndio kinywaji cha wapendwa na ndio dawa ya sumu kwa watenda madhambi.

قَدْ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٍ مَّشْرَبَهُمْ

“Kila wamoja wamejua mahali pale pa kunywea.”[2]

Hii leo tumekusukutueni kwa kinywaji cha shauku kilichochanganyikana na maji ya woga. Ninakuombeeni kwa jina la Allaah asisimame yeyote kutoka katika kikao hichi isipokuwa awe ametubu kwa Mkarimu na Mwingi wa kutunuku. Hakuna miongoni mwa wanywaji ambaye analia, anacheka, anacheza ala za muziki au amefungamana na watu? Hakuna miongoni mwa wanywaji ambao nafsi zao hazitulizani isipokuwa mpaka ataliki au apigwe upanga? Wengine mpaka walale. Vivyo hivyo juu ya wale wenye kunywa kinywaji cha mawaidha; wako ambao hulia juu ya madhambi yao, wengine hucheka kwa ajili ya kufikia yale matakwa yao, wengine kushikamana na msafara wa wanaoendelea na wako wengine ambao hawaridhiki mpaka waitaliki dunia mara tatu au waue matamanivu ya nafsi zao. Wengine wako kama wenye kulala na hawatambui chochote.

Je, wewe hii leo uko macho au umelala?

Vipi roho iliyodangana na iliyopotea inaweza kulala?

Lau kifua chako kingekuwa macho

basi macho yako yangelia

Kipindi cha usingizi wako mrefu

yamekaribia mambo makubwa yenye kutisha

Unafurahia yatayotokomea na umeshughulishwa na kifo

kama ambavo mlalaji anastarehe kwa ndoto yake nzuri

Michana yako imesahaulika na kupuuzwa

nyusiku zako unakuwa mwenye kulala na unapatwa na utwevu wa lazima

Umeshikilia yale ambayo utachukia matokeo yake

hivyo ndivo wanyama wanavyoishi duniani

Swalah na salamu zimwendee bwana wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake mpaka siku ya Qiyaamah na Allaah awawie radhi Maswahabah wote wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

سُبْحَانَ رَبِّكَ رَبِّ الْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ وَسَلَامٌ عَلَى الْمُرْسَلِينَ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

“Utakasifu ni wa Mola wako, Mola Mtukufu kutokamana na yale wanayomsifu, amani iwe juu ya Mitume na himdi zote ni stahiki ya Allaah, Mola wa walimwengu.”[3]

[1] 38:42

[2] 02:60

[3] 37:180-182

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dhamm-ul-Khamr, uk. 28-29
  • Imechapishwa: 03/08/2020