Swali: Myahudi na mnaswara ambaye amemwamini Mtume Wake na akamwamini Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapata ujira mara mbili. Je, hilo linapelekea yeye kuwa mbora kuliko mtu mmojammoja wa ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Haipelekei hivo. Allaah anaweza kumlipa thawabu mmoja katika ummah thawabu za ambaye amewaamini Mitume wote. Sisi tumewaamini Mitume wote (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Sisi tumewaamini na kuwasadikisha Mitume wote na tunataraji kupata mfano wa thawabu zao pamoja na thawabu za kumfuata kwetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu sisi tumewaamni Mitume wote na pia tunamwamini Allaah. Muislamu anawaamini Mitume wote na vitabu vyote vilivyoteremshwa kutoka mbinguni. Kwa hiyo kunatarajiwa kwake thawabu za kuwaamini Mitume hao wote.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22945/هل-يرجى-للمسلم-مثل-اجور-اتباع-بقية-الرسل
  • Imechapishwa: 21/09/2023