Thawabu 100.000 kwa misiki yote ya Makkah?

Swali: Kuswali katika msikiti Mtakatifu wa Makkah thawabu zake ni 100.000. Je, thawabu hizi zinahusu ule msikiti Mtakatifu au ni Makkah yote?

Jibu: Maoni sahihi ni Makkah yote. Baadhi ya wanazuoni wamefanya maalum kwamba ni pambizoni mwa Ka´bah. Maoni sahihi ni misikiti yote ya Makkah. Msikiti Mtakatifu umekusanya Makkah yote. Lakini kila ambavo msikiti utakuwa na waswaliji wengi ndio itakuwa bora. Pambizoni mwa Ka´bah ndio bora kutokana na wingi wa waswaliji, kule kuikaribia Ka´bah na kutoka nje ya makinzano ya wanazuoni. Lakini maoni sahihi ni kwamba inahusu misikiti yote ilioko Makkah mtu analipwa namna hiyo. Tunataraji kwake kuzidishiwa – Allaah akitaka. Hayo ndio maoni yaliyochaguliwa na Abul-´Abbaas Ibn Taymiyyah, Ibn-ul-Qayyim na kikosi cha Muhaddithuun.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4438/هل-كل-مكة-تعتبر-حرم
  • Imechapishwa: 17/06/2022