Mfanyakazi aliyepotea pasina mshahara wake

Swali: Kama nilikuwa na mfanyakazi anayenifanyia kazi na nikawa na kiwango cha pesa zake lakini hata hivyo simpati ili nimpe haki yake. Nimfanye nini?

Jibu: Ikiwa mtu anayo haki ya mwingine na amemkosa na hajui mahali alipo, amtolee nazo swadaqah kwa manuizi. Allaah atamfikishia thawabu zake. Namna hiyo dhimma yake itakuwa imetakasika. Akija baada ya kipindi fulani atampa khiyari; akitaka atakubali swadaqah aliyotolewa na thawabu zitakuwa zake, na akitaka atampa haki yake na thawabu zitamrudilia yeye.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4428/ما-حكم-من-عنده-حق-لانسان-فلم-يجده
  • Imechapishwa: 17/06/2022