Tayammum inachukua mahali pa maji

Twahara ya Tayammum inachukua nafasi ya maji. Twahara ya Tayammum haivunjiki isipokuwa kwa kuchenguka twahara ya aina ya maji au kuondoka udhuru wenye kuruhusu Tayammum.

Mwenye kufanya Tayammum kwa kukosa maji kisha [baadaye] akayapata, ni wajibu ajitwahirishe kwa maji. Allaah amefanya kujitwahirisha kwa udongo pale kunapokosekana maji. Watunzi wa Sunan wamepokea Hadiyth kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Udongo msafi ni wudhuu’ wa muislamu – au alisema ni twahara ya muislamu – hata kama hakupata maji kwa miaka kumi. Atapoyapata basi na amche Allaah na ajioshe nayo. Hakika hilo ni kheri.”[1]

[1] Abu Daawuud (333)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/365)
  • Imechapishwa: 15/05/2023