Kama mnavojua Jamaa´at-ut-Tabliygh wana mamilioni ya wafuasi. Wameenea katika ulimwengu wa Kiislamu na magharibi. Lakini hawana kile kiwango cha elimu ambacho anatakiwa kuwa nacho kila mlinganizi na khaswa ikiwa mlinganizi huyo analingania katika nchi za magharibi na nchi za makafiri. Hilo ni kwa sababu mambo yenye kutatiza na hoja tata zilizoko huko ni nyingi zaidi kuliko zilizoko katika nchi hizi. Kwa hivyo ikiwa si msomi wa Qur-aan na Sunnah basi hulazima kujibu kutokana na ujinga wake. Matokeo yake yeye mwenyewe anapotea na anasababisha watu wengi kupotea.

Kwa sababu hiyo mimi naona kuwa vijana wenye hamasa hii leo hakuna kiongozi wa kundi yeyote ambaye alikuwa msomi kwanza kabla ya kuwa kiongozi. Hili ndio tatizo la walinganizi wa leo katika ulimwengu wa Kiislamu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (1012)
  • Imechapishwa: 17/12/2020