Swali: Raafidhwah wamekuwa wengi katika nyumba za wanafunzi. Wameanza kutangamana na baadhi ya baadhi ya wanafunzi wanaotoka nje ya nchi na wana uchangamfu kwelikweli. Tutangamane nao vipi?

Jibu: Ikiwa wana uchangamfu kwenye kulingania katika Bid´ah zao, basi nyinyi mnatakiwa kuwa na uchangamfu mkubwa zaidi kwenye kulingania katika Sunnah. Allaah (´Azza wa Jall) amesema juu ya wafuasi wa haki wanapoisimamia kidete:

بَلْ نَقْذِفُ بِالْحَقِّ عَلَى الْبَاطِلِ فَيَدْمَغُهُ فَإِذَا هُوَ زَاهِقٌ

“Bali Tunavurumisha haki juu ya batili kasha inaisambaratisha.”[1]

Kule kuona kwetu uchangamfu wa Ahl-ul-Bid´ah juu ya Bid´ah zao – na khaswa zile Bid´ah kubwakubwa – kasha tunanyamaza au tunauliza nini tunachotakiwa kufanya, huo unazingatiwa ni woga. Ikiwa wao wako na ulinganizi, basi ulinganizi wenu nyinyi unatakiwa kuwa mkuu na mkubwa zaidi. Kwani nyinyi ndio mko katika haki na ni wenye kulipwa thawabu. Kuhusu Ahl-ul-Bid´ah wanapolingania katika Bid´ah zao ni wenye kupata dhambi na kuadhibiwa. Wataadhibiwa juu ya kila yule ambaye wamemlingania katika Bid´ah hizi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Na yule mwenye kulingania katika Uislamu msingi mbaya, basi anapata dhambi zake na dhambi za yule atakayeutenda mpaka siku ya Qiyaamah.”

Kwa hiyo mimi nakuhimizeni muwe na uchangamfu mkubwa zaidi. Ikiwa wao wanatoa pesa moja, basi nyinyi toeni pesa mbili. Ikiwa wanawaendea watu hawa katika nyumba zao na kufanya propaganda zao, basi nyinyi mnatakiwa kuwa na uchangamfu mkubwa zaidi juu jambo hilo.

[1] 21:08

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (24 A)
  • Imechapishwa: 17/12/2020