Tarawiyh ya mwanamke pamoja na wanamme msikitini

Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kuswali msikitini pamoja na wanamme swalah ya Tarawiyh?

Jibu: Ndio, inapendeza kufanya hivo ikiwa anachelea uvivu akiiswali nyumbani kwake. Vinginevyo nyumbani kwake ndio bora zaidi. Lakini ni sawa haja ikipelekea kufanya hivo. Wanawake walikuwa wakiswali na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) swalah tano. Lakini amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… lakini majumbani mwao ndio bora kwao.”

Lakini baadhi ya wanawake wanaweza kuhisi uvivu majumbani mwao na wakanyongeka. Ikiwa kutoka kwake kwenda msikitini hali ya kuwa wamejisitiri, wamevaa Hijaab na wamejiepusha kuonyesha mapambo na wamekusudia swalah na kusikiliza elimu, ni mwenye kulipwa thawabu kwa hilo. Ni malengo mazuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/18480/حكم-صلاة-المراة-التراويح-في-مسجد-الرجال
  • Imechapishwa: 10/04/2023