Kuirudia Witr iliyokutana na adhaana ya Fajr

Swali: Mara moja au mbili imetokea adhaana ya Fajr kunikuta huku ninaswali na wakati mwingine baada ya kutoa salamu adhaana inakuwa ndio inaanzwa. Je, niirudie Witr hii?

Jibu: Inatosha. Kwa sababu adhaana inatolewa kwa kudhania kuwa Fajr imeingia. Kukiadhiniwa na mtu yuko katika Witr atakamilisha. Hapana neno na inatosha kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/16336/هل-يعاد-الوتر-اذا-اذن-للفجر-اثناء-تاديته
  • Imechapishwa: 10/04/2023