Swali: Mwanamme akimtaliki mke wake ndani ya hedhi talaka inapita au haikupita?

Jibu: Ikiwa yeye mwanamme anajua hilo na mwanamke anajua hilo, maoni sahihi ni kwamba haipitiki kwa mtazamo wa baadhi ya wanazuoni. Wanazuoni wengi wanaona kuwa inapita. Lakini maoni sahihi zaidi ni kwamba haipiti kutokana na Hadiyth ya Ibn ´Umar. Hapo ni pale ambapo anajua kuwa ana hedhi.

Swali: Akiwa hajui?

Jibu: Inahesabika kwake. Kwa sababu hakuzua. Hakufanya uzushi. Akiwa anajua atakuwa amekusudia uzushi. Amekusudia uzushi na hivyo haihesabiki. Akiwa hajui au hakimu amehukumu hivyo basi talaka imepita. Mahakimu wengi wanahukumu kupita kwake. Maoni sahihi zaidi, japo ni ya wanazuoni wachache, ni kwamba haipiti. Wanazuoni wengi wanaona kuwa inahesabika. Kwa sababu Ibn ´Umar alijihesabia nayo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22050/ما-حكم-طلاق-الحاىض
  • Imechapishwa: 20/10/2022