Swali: Je, inafaa kuingiza video, TV na zana za picha ndani ya msikiti?

Jibu: Hapana, haijuzu. Huku ni kuingiza maovu. Kitendo cha yeye kuwasha redio na ndani yake kukawa kuna kitu katika nyimbo au sauti za madhambi.

Swali: Baadhi ya watu wanajengea hoja ya kufaa kwa kuwepo zana za picha katika msikiti wa Makkah.

Jibu: Hapana, haifai kufanya hivo. Kitendo chao sio hoja. Picha ni haramu kabisa.

Swali: Hata katika msikiti Mtakatifu?

Jibu: Katika msikiti Mtakatifu pia zimekatazwa. Wasimamizi wakichukulia wepesi jambo hilo haijakuwa ni dalili. Kuchukua wepesi mwenye kuchukulia wepesi haiwi hoja.

Swali: Baadhi ya watu wanasema kuhusiana na mashine ulizozitaja punde kidogo kwamba vitu hivyo vinanufaisha ulinganizi na vinawanufaisha watu.

Jibu: Hapana, hapana. Ni sawa ikiwa ni jambo jema peke yake kama vile redio ya Qur-aan. Lakini ndani yake kunaweza kuingizwa matangazo ya vitu visivyokuwa vizuri. Hata hivyo ni sawa ikiwa vitahifadhiwa na mtu akawa anasikia redio ya Qur-aan au vitu vizuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22048/حكم-ادخال-الات-التصوير-والفيديو-الى-المسج
  • Imechapishwa: 20/10/2022