Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

Amesema (Ta´ala):

“Mola Wako anastaajabu kwa kijana asiyehadaika na mambo ya kipuuzi na matamanio.”[1]

MAELEZO

11 – Kustaajabu. Kustaajabu kwa Allaah ni miongoni mwa sifa Zake zilizothibiti kwa Qur-aan, Sunnah na maafikiano ya Salaf. Allaah (Ta´ala) amesema:

بَلْ عَجِبْتَ وَيَسْخَرُونَ

“Bali umestaajabu ilihali wao wanafanya dhihaka.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mola Wako anastaajabu kwa kijana asiyehadaika na mambo ya kipuuzi na matamanio.”

Salaf wameafikiana juu ya kumthibitishia Allaah kustaajabu. Kwa hiyo ni lazima kumthibitishia nayo pasi na kuipotosha, kuikanusha, kuifanyia namna wala kuipigia mfano. Ni kustaajabu kikweli ambako kunalingana na Allaah.

Ahl-ut-Ta´twiyl wamefasiri kuwa ni kulipa. Tunawaraddi kwa yale yaliyokwishatangulia katika kanuni ya nne. Kuna aina mbili za kustaajabu:

1 – Kustaajabu kwa yule mwenye kustaajabu kujificha na sababu ya chenye kustaajabisha. Tahamaki anastaajabu na kushangaa pale anapokiona kitu hicho. Aina hii haiwezekani kabisa kwa Allaah. Hakuna chochote kinachofichikana kwa Allaah.

2 – Kustaajabu iwe kunatokamana na kitu kutoka katika mazowea yake au vile kinavyotakiwa kuwa ilihali yule mwenye kustaajabu awe na ujuzi juu ya kitu hicho. Aina hii ndio yenye kuthibiti kwa Allaah (Ta´ala).

[1] Ahmad (4/151), Ibn Abiy ´Aaswim (1/250), Abu Ya´laa (1479), at-Twabaraaniy katika “al-Kabiyr” (17/309), al-Haythamiy (10/270) na wengine. Imaam al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) amesema kuwa ni dhaifu katika ”as-Silsilah adh-Dhwa´iyfah” (2426). Lakini Hadiyth iliyopokelewa na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ”Allaah anastaajabu na fulani na fulani… ” ni Swahiyh. (Tazama Swahiyh al-Bukhaariy (4889)).

[2] 37:12

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 58-60
  • Imechapishwa: 20/10/2022