33. Kumthibitishia Allaah kushuka katika mbingu ya chini

Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

Katika Sunnah Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mola Wetu (Tabaarak wa Ta´ala) huteremka kila usiku katika mbingu ya chini.”[1]

MAELEZO

10 – Kushuka. Kushuka kwa Allaah katika mbingu ya chini ni miongoni mwa sifa Zake zilizothibiti kwa Sunnah na maafikiano ya Salaf. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mola wetu hushuka katika mbingu ya chini pale kunapobaki theluthi ya mwisho ya usiku na husema: “Ni nani mwenye kuniomba du´aa nimuitikie… “[2]

Kuna maafikiano juu yake.

Salaf wameafikiana juu ya kumthibitishia Allaah kushuka. Kwa hiyo ni lazima kumthibitishia nayo pasi na kupotosha, kukanusha, kuufanyia namna wala kuupigia mfano. Ni kushuka kikweli ambako kunalingana na Allaah.

Ahl-ut-Ta´twiyl wamefasiri kuwa ni kushuka kwa amri Yake, rehema Zake au Malaika miongoni mwa Malaika Zake. Tunawaraddi kwa yale yaliyokwishatangulia katika kanuni ya nne. Ipo njia ya nne ambayo ni kwamba amri na makatazo hayawezi kusema:

“Ni nani mwenye kuniomba du´aa nimuitikie… “

[1] al-Bukhaariy (1145) na (6321) na Muslim (758).

[2] al-Bukhaariy (1145).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 58
  • Imechapishwa: 20/10/2022