Talaka wakati mwanamke yuko na hedhi

Swali: Talaka wakati mwanamke yuko katika hedhi inahesabiwa?

Jibu: Inahesabiwa. Akimtaliki mara tatu kunapita. Hata hivyo anapata dhambi kwa kufanya hivo. Ikiwa ana haki ya kumrudi, afanye hivo. Kama hana haki ya kufanya hivo anatalikika na anajitenga naye. Aidha anapata dhambi kwa kufanya hivo. Kuhusu talaka yenyewe inapita. Inapita japokuwa ni haramu. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kumwambia Ibn ´Umar:

“Mwamrishe amrejee.”

Kumrudi hakukuwi isipokuwa kwa talaka iliyopita. Ingekuwa talaka haikupita asingemwambia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amrejee mwanamke yule.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (7) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–15041434.mp3
  • Imechapishwa: 16/12/2016