Talaka tatu kwa mpigo zinahesabika ni tatu

Swali: Mwanaume akimtaliki mke wake mara tatu kwa mpigo mmoja – je, inahesabiwa ni talaka moja au talaka tatu?

Jibu: Kikosi kikubwa cha wanazuoni kinaona kuwa inahesabiwa ni talaka tatu. Hivo ndivo yanavosema madhehebu. Wakati wa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) wakati alipoona watu wanachukulia wepesi suala la talaka, alipitisha talaka tatu zinazopigwa kwa mpigo mmoja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (38)
  • Imechapishwa: 29/06/2023