Ndio maana Jamiylah alijivua kutoka kwa Thaabit bin Qays

Swali: Wakati mwanaume alipomweleza mke wake kuwa anataka kuongeza mke, akamuomba kujivua katika ndoa au kutalikiwa kwa kujengea hoja maneno ya Thaabit bin Qays (Radhiya Allaahu ´anhaa):

”Ee Mtume wa Allaah! Sina cha kumlaumu upande wa tabia wala dini, lakini mimi nachukia kufuru baada ya Uislamu.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Je, utarudishia shamba lake?” Akasema: ”Ndio.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Kubali shamba na mtaliki.”[1]

Je, anayo haki ya kuomba jambo hilo?

Jibu: Yeye alikuwa akimchukia. Alikuwa anamchukia kwa sababu Thaabit bin Qays (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa mbaya. Hakuwa anaweza kumwangalia. Alikuwa (Radhiya Allaahu ´anh) mbaya. Akasema kuwa anachukia kukufuru baada ya Uislamu kwa sababu havutiwi naye na akachelea asimuasi na matokeo yake akaingia Motoni. Hapo ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwamrisha kumwacha huru.

[1] al-Bukhaariy (5273).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (38)
  • Imechapishwa: 29/06/2023