Bora mtu kufanya alichokiapia au kutokukifanya?

Bora kwa mtu kufanya kitu alichokiapia kuwa hatofanya au bora ni kukifanya? Kwa mfano mtu akiapa “naapa kwa Allaah sintomsemesha fulani” ilihali ni muislamu, uchaji Allaah zaidi ni wewe kumsemesha. Kumsusa muislamu ni haramu. Msemeshe na utoe kafara kwa kiapo chako. Kwa sababu hili ndio linamridhisha Allaah zaidi. Mfano mwingine lau utasema “naapa kwa Allaah sintomtembelea ndugu yangu”. Katika hali hii tunasema kumtembelea ndugu ni kuunga kizazi. Kuunga udugu ni jambo la wajibu. Mtembelee ndugu yako na utoe kafara juu ya kiapo chako. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote ayakayeapa yamini kisha akaona linalomridhisha Allaah zaidi kuliko alichokiapia, basi akafirie kiapo chake na afanye lile linalomridhisha Allaah zaidi.”[1]

Ufupisho ni kuwa kuapa kwa kitu kilichopita mtu asiulize kwa kuwa hakina kafara. Lakini ima mwapaji akawa amesalimika au mwenye kupata madhambi. Ikiwa amesema uongo basi ni mwenye kupata dhambi. Na ikiwa amesema ukweli basi ni mwenye kusalimika.

[1] Muslim (1651).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/533)
  • Imechapishwa: 29/06/2023