Kiapo juu ya jambo linalokuja huko mbele[1] ndio kiapo kilicho na kafara. Mtu akiapa ju ya kitu kinachokuja mbele na akaenda kinyume na kitu hicho alichokiapia, basi ni wajibu kwake kutoa kafara. Isipokuwa ikiwa kama ataapa na kusema “Akitaka Allaah” katika hali hii hana kafara juu yake hata kama hatofanya kitu hicho [alichokiapia].

[1] https://firqatunnajia.com/bora-mtu-kufanya-alichokiapia-au-kutokukifanya/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/533 )
  • Imechapishwa: 29/06/2023