Swali: Baadhi ya watu wamewakufurisha Ashaa´irah na wametumia hoja maneno ya Ibn Qudaamah katika “al-Mughniy” na al-Harawiy. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Wanachuoni wanaonelea kuwa Ashaa´irah ni Ahl-ul-Bid´ah. Wakati Muhammad bin ´Aliy as-Swaabuuniy alipoandika makala kuhusu kwamba Ashaa´irah ni katika Ahl-us-Sunnah, Shaykh al-Fawzaan na Shaykh Ibn Baaz walimraddi. Kwa ufupisho Ashaa´irah ni Ahl-us-Sunnah ni kwa yale wanayokubaliana na Ahl-us-Sunnah na sio Ahl-us-Sunnah kwa yale wanayoenda kinyume na Ahl-us-Sunnah. Wakasema kuwa ni Ahl-ul-Bid´ah kwa yale wanayoenda kinyume na Ahl-us-Sunnah. Hawakuwakufurisha. Ni kweli mtu anaweza kusema kuwa wana fikira za kikafiri, lakini hawakuwakufurisha. Hali yao ni kama ya Ahl-ul-Bid´ah wengine; Takfiyr haifanywi kwa watu wao binafsi isipokuwa mpaka baada ya kusimamiwa na hoja na kuondosha utata wao – na Allaah ndiye Aajua zaidi.

Wanafunzi wasipetuke mipaka katika Takfiyr na kuingilia suala hili. Masuala haya warejee kwa wanachuoni wakubwa, kama alivyotanabahisha hilo mwandishi mwanzoni wa kijitabu hichi na vilevile mimi – na Allaah ndiye Anajua zaidi.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin´Umar Baazmuul
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=146687
  • Imechapishwa: 11/04/2015