Swali: Kuna baadhi ya watu wanaosema “Irehemu Salafiyyah na wala usiifarikanishe kwa kuita Haddaadiyyah na kadhalika”. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Maneno haya yanakwenda kinyume na Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya kwamba Ummah huu utagawanyika makundi sabini na tatu na kwamba yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio alosema kuwa ni makundi na na kwamba yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu. Wanachuoni wanasema maneno ya Mtum “Yote yataingia Motoni isipokuwa moja” ni matishio. Bi maana hii ndio adhabu yao ikiwa Allaah Atapenda Kuwaadhibu na Akipenda Atawasamehe. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kuwa kutatokea makundi na yatafika sabini na tatu katika Ummah. Vipi basi utawahukumu Salafiyyuun ya kwamba wamewagawanya watu katika mapote, tofauti na makundi yanayooenda kinyume na Uislamu?

Wakati Shaykh Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd alipotaka kuandika kitabu “Tasniyf-un-Naas bayn adh-Dhann wal-Yaqiyn” nilizungumza naye. Alizungumza (Rahimahu Allaah) na mimi kabla ya kufa na kabla ya kuchapisha kitabu. Shaykh akanieleza kuwa atachapisha kitabu kinachoitwa “Tasniyf-un-Naas bayn adh-Dhann wal-Yaqiyn”. Nikamwambia kuwa kicha cha khabari sio cha sawa kwa sababu msemo huo unatolea ishara kama vile unawakemea kuwagawanya watu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio aliyesema:

“Na Ummah huu utagawanyika katika makundi sabini na tatu.”

Nikamwambia awe makini na muwazi ikiwa kama atalazimika kukiandika. Nimamweleza maneno aliyosema ash-Shaatwibiy katika “al-I´tiswaam” na wanachuoni wengine juu ya mambo haya. Wanachuoni wamesema kuwa ni sawa kuwaita na kuwaeleza wafuasi wa mapote ili kuwatahadharisha watu na Bid´ah zao, utata wao na hali zao. Je, si ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) ndiye alisema kumwambia mwanamke alouliza kama anapaswa kulipa Swalah:

“Je, wewe ni Haruuriyyah?”?

Je, ´Aaishah anataka kuwagawanya watu?

Wakati Taabiy´iyyaani wawili walipokuja kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na kumuuliza kuhusu Ahl-ul-Qadr na wanatumia jina la “Ahl-ul-Qadr”. Ibn ´Umar akamkubalia kwa jina hilo na kusema:

“Waambie kuwa mimi niko mbali na wao.”

Walipewa jina “Ahl-ul-Qadr”. Namna hii ndivyo ilivyokuwa uanisho, jina na wasifu wa wenye kwenda kinyume. Sisi tunapita katika njia hii kwa sababu ni njia ya waumini. Mgawanyiko na tofauti iliyopo katika Ummah huu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliuelezea. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitaja baadhi ya mapote haya na kusema ikiwa ni pamoja na:

“Khawaarij ni mijibwa ya Motoni.”

Aliwaita kuwa ni “Khawaarij”.

Akasema:

“Qadariyyah ni waabudu moto wa Ummah huu.”

Akawaita kuwa ni “Qadariyyah”.

Watu wote wenye mfarakano waenda kinyume sisi tutawaita, kuwasifu na kuwaelekezea kidole ikiwa hakuna njia nyingine ya kutahadharisha Bid´ah zao na kuzitokomeza isipokuwa kwa kutumia njia hii tu. Hakuna tatizo kwa hilo. Hilo haliwafarikanishi watu. Linawafanya watu kuwa na umoja katika haki. Je, hujui kuwa Kitabu walichoteremshiwa Waislamu kinaitwa “al-Furqaan” kwa sababu kinapambanua baina ya haki na batili? Je, hujui kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitenganisha kati ya mtoto na baba yake, mtu na ndugu zake? Kwa sababu anatenganisha kati ya waumini na makafiri. Hali kadhalika na sisi tunatenganisha kati ya Ahl-us-Sunnah na Ahl-ul-Bid´ah na wale wenye kujifarikisha na wale wenye kujiweka umoja. Hili haliwadhuru watu. Haliwafarikanishi watu. Linawafanya watu kuwa na umoja – na Allaah ndiye Anajua zaidi.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin´Umar Baazmuul
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=146687
  • Imechapishwa: 11/04/2015