Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy – mkosoaji mchanganyikiwaji?

Swali: Ni ipi nasaha yako kwa vijana huku kwetu Marocco wanaoeneza utata juu ya Shaykh Rabiy´? Mara wanasema kuwa ni mzee alochanganyikiwa. Mara wanasema kuwa kazi yake ni kuraddi tu. Mara wanasema kuwa ni mzee sana.

Jibu: Kitu cha kwanza sio mzee kiasi hicho mpaka kufikia kuchanganyikiwa. Nijuavyo ni kwamba ni mdogo kwangu. Alichukua shahada ya chuo kikuu kwenye kitivo cha Shari´ah karibu miaka mine baada yetu. Nijuavyo katika maneno yake ni kuwa hana makosa yoyote katika ´Aqiydah yake wala elimu. Anatilia juhudi kubwa kuwaraddi wale anaoonelea wanaenda kinyume. Ni jambo lisilokuwa na shaka ya kwamba pale ambapo Shaykh anapopata tu taarifa juu ya mtu anayeeneza elimu na akaona kosa lake ambalo haliwezi kunyamaziwa. Katika hali hiyo ni wajibu kwake kuweka wazi lile analolijua. Sijaona kosa lolote katika ´Aqiydah yake.

Kuhusiana na kwamba ana mtazamo wa kimakosa katika imani, sijui kuwa anakanusha imani ya kimatendo. Uhakika wa mambo ni kwamba ni mwenye kupupia kufafanua imani kwa mujibu wa Salaf kama Maalik, ash-Shaafi´iy, Ahmad na Abu Haniyfah. Hawa wote ni maimamu wa kheri na wa elimu.

Wakati mwanachuoni anamkosoa mwanachuoni mwingine, ni jambo lenye kujulikana ya kwamba kunaweza kuwepo ugomvi kati ya wanachuoni. Ndio maana ni katika mfumo wa kielimu kutochukua maneno ya wagomvi wawili wanayotupiana. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah ana kijitabu kidogo kinachoitwa “Raf´-ul-Malaam ´an A-immat-il-A´alaam”.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=146694
  • Imechapishwa: 11/04/2015