Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Liharakisheni jeneza. Akiwa mwema, basi ni kheri mnayomtangulizia, na akiwa kinyume na hivo, basi hiyo ni shari mnayoiondoa kutoka kwenye shingo zenu.”[1]

Hadiyth pia inahimiza kutilia umuhimu jambo la nduguyo muislamu, ni mamoja yuhai au ameshakufa, na kumuharakisha katika yale yenye kheri na yeye katika dini na dunia yake. Sambamba na hilo Hadiyth pia inahimiza kujiweka mbali na yale yote yanayopelekea katika shari na kuwatenga mbali wahalifu, kukiwemo zile hali ambazo mtu anapewa majaribio katika kuchanganyikana nao.

[1] al-Bukhaariy (1315) na Muslim (944).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bahjat-ul-Abraar, uk. 97
  • Imechapishwa: 26/02/2021