Swali: Kuna mwanamke amechora Suurat Yuunus (´alayhis-Salaam) kwa batili. Wakati Allaah (Ta´ala) anasema:

أَنَّ لَهُمْ قَدَمَ صِدْقٍ عِندَ رَبِّهِمْ

“… kwamba watapata cheo kitukufu mbele ya Mola wao.” (10:02)

anachora mguu. Wakati Allaah (Ta´ala) anasema:

ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“Kisha akalingana juu ya ´Arshi.” (10:03)

anachora kiti. Ameichora Suurah yote namna hii.

Jibu: Hili halijuzu. Haijuzu kuifasiri Qur-aan kwa mapicha haya. Unachora kwa mujibu wa ufahamu wako?

أَنَّ لَهُمْ قَدَمَ صِدْقٍ عِندَ رَبِّهِمْ

“… kwamba watapata cheo kitukufu mbele ya Mola wao.” (10:02)

Hufahamu wala mguu wa mwanaadamu. Makusudio sio hayo. Unaweza kuifasiri Qur-aan kimakosa na ukazungumza juu ya Allaah pasina elimu. Qur-aan isifasiriwe kwa mapicha. Kwa ajili hiyo ndio maana wanacuoni wameikataa Tafsiyr ya Qur-aan ya Tantawiy Jawhariy[1] mmisri. Anajulikana. Anafasiri Aayah za Qur-aan kwa mapicha. Hili halijuzu.

[1] Tazama http://www.tantawi-gawhari.net/

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/nawaqid-18-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/04/2015