Watu wa dini wenye kuvaa nguo za kubana

Swali: Kuna watu wengi wenye msimamo Ulaya wanavaa suruwali zenye kuachia na juu yake wanavaa mashati ya kubana yanayoonesha viungo vyao ambayo yanawatia kwenye mitihani wasichana. Wanaponasihiwa wanasema kuwa ´Awrah ni kati ya kitovu na magoti. Ni ipi nasaha yako?

Jibu: Ni kweli ya kwamba ´Awrah ni kati ya kitovu na magoti, lakini wakivaa mavazi yenye kubana hili ni jambo lingine. Ni fitina nyingine. Mtu asivae mavazi yenye kubana yanayowatia wengine kwenye mitihani. Mtu anakuwa amefunika ´Awrah yake, lakini amefunika kwa kitu chenye kufitinisha. Wafunike kwa mavazi yenye kuachia. Mavazi ya kubana yanazidisha tu fitina.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/nawaqid-18-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/04/2015