Mavazi ya kubana kwa wanawake ni fitina zaidi kuliko kuwa uchi

Swali: Watu wengi wanazungumzia mavazi ya kubana ya mwanamke na ya kuonesha na wanaonelea kuwa maadamu mavazi yanaonesha viungo vyake kama miguu yake, kifua chake na tumbo lake ni katika mavazi yenye kuheshimika.

Jibu: Hapana, sio mavazi yenye kuheshimika. Haya yana fitina zaidi kuliko kuonesha viungo vyake visivyotakikana kuonekana (´Awrah). Mavazi ya kubana yanayoonesha viungo vya siri vya mwili ni fitina zaidi kuliko kuwa uchi. Mwanamke anaweza kuwa mbaya na asiyevutia, lakini pale tu anapovaa mavazi kama haya anakuwa ni fitina na kuonekana ni mzuri. Haifai kwake kuvaa hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/nawaqid-18-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/04/2015