Swali: Je, inajuzu kwa bibiharusi kuvaa geuni nyeupe ya biharusi siku ya harusi au huku ni kujifananisha na makafiri?

Jibu: Mavazi inategemea na desturi ya jamii. Usiende kinyume na mavazi ya jamii. Ukienda kinyume na mavazi yao ni mwenye kutaka kuonekana. Isipokuwa tu pale ambapo mavazi ya jamii ni haramu. Kimsingi ni kwamba mavazi ni yenye kuruhusiwa mpaka pale yatapokwenda kinyume na dalili. Katika hali hiyo yatakuwa ni haramu. Lakini muda wa kuwa hakuna dalili ya kuonyesha kuwa ni haramu na watu wamezowea kuvaa mavazi haya na wanawake wana mavazi yao na wanaume wana mavazi yao [itakuwa ni sawa]. Mavazi ni katika mambo ya desturi. Hayapingwi midhali hayaendi kinyume na dalili ya Kishari´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/nawaqid-18-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/04/2015