Swawm ya Ramadhaan Makkah ni sawa na swawm elfu mahali kwengine?

Swali: Kufunga Ramadhaan Makkah ni sawa na kufunga miezi elfu maeneo mengine? Je, Hadiyth hii ni Swahiyh?

Jibu: Si Swahiyh. Kumepokelewa juu ya hilo Hadiyth dhaifu ambayo haikusihi. Kilichothibiti ni katika swalah peke yake. Kuswali katika msikiti Mtakatifu ni sawa na swalah laki moja katika msikiti mwingine na kuswali katika msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni bora kuliko swalah elfu moja mahali kwengine. Kuhusu swawm hakukuthibiti kitu zaidi ya Hadiyth dhaifu na kwamba ni bora kuliko swalah laki moja ukilinganisha na maeneo mengine. Hata hivyo ni dhaifu. Lakini matendo mema yana fadhilah ya kipekee Makkah. Swawm, swadaqah, Adhkaar na matendo mengine mema yana fadhilah ya kipekee. Hata hivyo hakuna dalili inayobainisha kiwango fulani isipokuwa swalah peke yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/19990/ما-صحة-حديث-صوم-رمضان-في-مكة-يعدل-صيام
  • Imechapishwa: 20/03/2023