Kusimama kunakofaa na kusikofaa

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kuwaambia Maswahabah:

“Msimamieni bwana wenu.”

Wakasimama kwa ajili yake, wakampokea na kumsalimia. Kuna tofauti kati ya kusimama huku na huku. Kinachochukiza ni kusimama kwa ajili yake ilihali ameketi chini na si kwa ajili ya kupeana naye mkono na mazungumzo. Bali unasimama kwa ajili yake namna hii. Hili ndio linalochukiza. Unamsimamia kwa ajili ya kumtukuza. Ni kitu kisichojuzu kwa sababu ni katika matendo ya waajemi. Hata hivyo ni jambo linakubalika katika Shari´ah kusimama kwa ajili ya kumpokea, kupeana naye mkono, kumshika mkono, kumkalisha mahali pako au mahali pengine. Hili la pili limefanywa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na likafanywa na Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya hivo kwa msichana wake alipoingia, akamsimamia na akamshika mkono. Vilevile anapoingia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mahali alipokuwa msichana wake basi anamsimamia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1749/لفرق-بين-القيام-للقادم-والقيام-الى-القادم
  • Imechapishwa: 20/03/2023