Swawm ya Nabii Daawuud siku ya ijumaa

Swali: Vipi ikiwa mtu anafunga siku moja na anakula siku ya kufuata na swawm yake ikakutana na siku ya ijumaa?

Jibu: Afunge siku ya ijumaa na afungue siku ya jumamosi. Hakufunga kwa sababu ya siku ya ijumaa. Amefunga kutokana na kanuni inayosema: anafunga siku moja na kufungua siku inayofuata.

Swali: Vipi ikiwa analo deni la kulipa?

Jibu: Afunge siku ya ijumaa. Hiyo ni swawm inayomlazimu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22796/حكم-الجمعة-لمن-يصوم-يوما-ويفطر-يوما
  • Imechapishwa: 25/08/2023