Swawm kwa mgonjwa wa vidonda vya tumboni

Swali: Mama yangu ana vidonda vya tumboni na daktari amemshauri asifunge isipokuwa baada ya miaka miwili au miaka mitatu. Baada ya hapo ndipo ataanza kufunga kila wiki siku mbili peke yake na kadhalika mpaka pale itapoboreka hali yake. Ni ipi hukumu?

Jibu: Allaah amemuwekea mgonjwa Shari´ah ya kula. Amesema (Ta´ala):

وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

”Na atakayekuwa mgonjwa au safarini basi [atimize] idadi katika siku nyinginezo.”[1]

Ikithibiti kwa kauli ya daktari muaminifu au madaktari waaminifu ya kwamba maradhi haya ya ndani yanamdhuru iwapo atafunga, basi hapana neno kula. Ategemee maneno ya daktari mwaminifu. Akihakikisha kwa madaktari wawili itakuwa kamili na vyema zaidi. Wakithibitisha kuwa swawm inamdhuru kutokana na vidonda vya tumboni au maradhi mengine, basi ale  na kufanya hivo ndio bora kwake. Baada ya hapo atalipa na hakumdhuru kitu.

[1] 02:185

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/7451/حكم-افطار-رمضان-لمن-اصيب-بالقرحة
  • Imechapishwa: 25/03/2023