Swali: Je, kusimama usiku ilikuwa lazima kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Wako wanazuoni waliosema hivo. Kuna makinzano kati ya wanazuoni. Kwa sababu Allaah amesema:

وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ

“Amka sehemu ya usiku na uswali… “[1]

ni amri. Hii inajulisha ulazima. Wengine wakasema ni kwa njia ya mapendekezo. Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoulizwa:

“Je, kuna kinachonilazimu zaidi ya swalah tano?” Akajibu: “Hapana, isipokuwa ukijitolea.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaingia ndani ya maamrisho.

[1] 17:79

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/6690/هل-كان-قيام-الليل-واجبا-على-النبي-ﷺ
  • Imechapishwa: 11/04/2023