Swali: Ni ipi hukumu ya anayepinga adhabu moja wapo miongoni mwa adabu za Allaah, kama vile adhabu ya mwenye kuritadi, kwa sababu eti hakuna kulazimishana katika dini na kwamba hakuna dalili ya hilo?

Jibu: Adhabu ya kuritadi haihusiani kitu na kumlazimisha mtu katika dini. Ni kwa sababu ya kuheshimisha dini ya Allaah na isichezewe. Matokeo yake ikawa watu wanasilimu, kisha wanaritadi, wanasilimu na kujua kuwa Uislamu ndio haki, kisha wanaritadi. Huyu anauliwa kwa sababu anafanya mchezo na dini ya Allaah na sio kwa sababu eti ya kurejea katika Uislamu. Hakuna mtu anayelazimishwa kuingia katika Uislamu. Inahusiana na kuingia. Hakuna yeyote anayelazimishwa kuingia. Lakini akitoka katika dini na akaritadi analazimika kuuliwa kwa sababu ni mhalifu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 11/04/2023