Swalah ya Shuruuk ndio swalah ya Dhuhaa

Swali: Rak´ah mbili zinazokuwa baada ya kuchomoza jua ni lazima kunuia kuwa ni swalah ya Dhuhaa?

Jibu: Hata kama hakuniua kuwa ni Dhuhaa, inahesabiwa kuwa ni Dhuhaa. Hata hivyo kuswali Rak´ah zingine wakati jua limepanda juu kidogo ni bora zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali Rak´ah nane. Kwa hivyo akiswali Rak´ah nane, sita au nne kunapendelewa zaidi.

Swali: Vipi kuhusu Hadiyth inayoeleza kuwa thawabu zake ni kama za Hijjah na ´Umrah?

Jibu: Hadiyth hiyo haina neno na njia zake ni nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24884/ركعتا-الشروق-هل-ينوي-بهما-الضحى
  • Imechapishwa: 27/12/2024