Ni lipi bora katika kukusanya Witr na Shufwa?

Swali: Je, ni bora kuunganisha Witr na Shufwa au kuahirisha Shufwa hadi mwisho wa usiku? Kwa mfano mtu akiswali Shufwa mwanzoni mwa usiku kisha akapenda kuahirisha Witr hadi mwisho wa usiku. Je, azitenganishe na kuswali Witr peke yake mwishoni?

Jibu: Jambo ni lenye wasaa na sijui kosa lolote kuhusu hilo. Lakini ikiwa ataweza kuswali Witr pamoja na Shufwa mwishoni mwa usiku, hilo ni bora zaidi kwa sababu swalah ya mwisho wa usiku ina fadhilah zaidi. Ikiwa itawezekana, anaweza kuahirisha Shufwa pamoja na Witr kwa kuswali Rak´ah mbili au nne mwishoni mwa usiku au Rak´ah tano au tatu kwa pamoja. Hii ni bora zaidi kwa sababu inazidisha thawabu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24883/ما-الافضل-في-جمع-الوتر-مع-الشفع
  • Imechapishwa: 27/12/2024