Bora kurefusha kisimamo cha usiku au kuongeza idadi ya Rukuu´ na Sujuud?

Swali: Kipi ni bora zaidi; kusimama kwa muda mrefu katika swalah au kuongeza idadi ya Rukuu´ na Sujuud?

Jibu: Kusimama kwa muda mrefu ni bora zaidi, kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hata hivyo asijifanyie ugumu. Ikiwa mtu atahisi uzito, basi afanye kati na kati na kuongeza idadi ya Rukuu´ na Sujuud. Hivo ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24887/هل-طول-القيام-افضل-ام-الركوع-والسجود
  • Imechapishwa: 27/12/2024