Sujuud kwa anayetaka kumuomba Allaah

Swali: Ikiwa mtu anataka kuomba du´aa nje ya swalah inafaa asujudu ili awe karibu zaidi na Allaah?

Jibu: Aombe du´aa wakati wa Sujuud, ni kitu kinachopendeza. Ni moja ya sababu za kukubaliwa kwa du´aa.

Swali: Je, hili linafaa nje ya swalah?

Jibu: Hapana, hapana. Kufanya sijda peke yake nje ya swalah haijawekwa katika Shari´ah. Sujuud imesuniwa ndani ya swalah au kutokana na sababu maalum kama vile sijda ya kushukuru au sijda ya kisomo. Au kufanya ´ibaadah kwa kusujudu peke yake si jambo limewekwa katika Shari´ah. Makusudio alipomwambia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amsaidie kwa kusujudu kwa wingi maana yake ni kuswali kwa wingi. Hayo ndio makusudio yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24888/هل-يشرع-ان-يسجد-من-اراد-ان-يدعو-الله
  • Imechapishwa: 27/12/2024