Swalah ya mzee anayepotewa na akili anaposwali

Swali: Kuna mwanamke mwenye umri mkubwa anasahau sana hivi karibuni ambaye hapo mwanzoni alikuwa ni mtu wa ´ibaadah na wema. Kipindi cha mwaka na nusu au takriban miaka miwili hatawadhi isipokuwa mpaka apelekwe bafuni. Wakati mwingine anafanya Tayammum kwenye kitanda chake. Haswali isipokuwa mpaka akumbuke. Na anaposwali anasahau na anazungumza ndani ya Swalah na yule aliyeko pembezoni mwake. Wakati mwingine huenda hata akaimba mashairi ilihali yuko anaswali. Tufanye nini na yeye na juu yake ana kitu?

Jibu: Lililo dhahiri ni kwamba mwanamke huyu amechanganyikiwa na akili zake zimemuondoka. Dalili ni kule kuimba mashairi na yeye yuko anaswali. Huyu haandikiwi dhambi. Mtu akichanganyikiwa mwishoni wa uhai wake, mwendawazimu au mtoto mdogo, ´ibaadah haimuwajibikii. Haimlazimu swalah wala swawm.

Lakini ikiwa ni mtu ambaye akili zake zinaondoka na zinarudi, pale ambapo akili zake zinamrudi alazimishwe kuswali kwa kumwambia aswali. Hivyo atatawadha na kuswali. Pale ambapo anakuwa hana akili, hana juu yake swalah wala swawm.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4734
  • Imechapishwa: 17/11/2014