Wajibu kwa mwanafunzi anayenufaika na elimu kwenye kanda

Swali: Kuhusiana na mwanafunzi akisoma vitabu na maelezo yake kwenye kanda ya kusikiliza. Je, mtu kama huyu anazingatiwa kuwa ni katika watafutaji wa elimu?

Jibu: Atafaidika. Lakini hata hivyo hili halitoshelezi. Ni lazima kwake kuhudhuria mizunguko ya kielimu. Ni lazima kwake kuwauliza wanachuoni. Ni lazima kwake vilevile kusoma vitabu [kwa wanachuoni]. Lakini ikiwa hakupata urahisi wa kufanya hivo asikilize kanda zenye faida na anufaike kwayo, ahudhurie duruus, aulize juu ya yale yenye kumtatiza na awasiliane na wanachuoni. Ni lazima ajumuishe baina ya mambo yote haya. Asitosheke na kanda tu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4734
  • Imechapishwa: 17/11/2014