Swali: Je, tuwafanyie Takfiyr Rawaafidhw wote kwa jumla na mapote yao yanayoabudu makaburi?

Jibu: Mwenye kufanya Shirki na ameshasimamishiwa hoja anakufurishwa. Ni lazima afanyiwe Takfiyr. Asiyewakufurisha washirikina au akawa na shaka juu ya ukafiri wao au akaonelea kuwa madhehebu yao ni sahihi, basi yeye pia ni kafiri kama wao. Ni moja katika mambo yanayovunja Uislamu wa mtu. Miongoni mwa mambo yanayovunja Uislamu wa mtu ni kutowakufurisha washirikina, kuwa na shaka juu ya ukafiri wao au kuonelea kuwa madhehebu yao ni sahihi. Mwenye kufanya Shirki, kama mfano wa kuomba mwingine asiyekuwa Allaah, kama Rawaafidhw ambao wanawaabudu Ahl-ul-Bayt badala ya Allaah, au wanamkadhibisha Allaah kwa kuwatakasa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum), au [sauti haisikiki], huku ni kuritadi na kutoka katika Uislamu. Atafanyiwa Takfiyr baada ya kusimamishiwa hoja.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4734
  • Imechapishwa: 17/11/2014